KARIBU ATAPE
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadventista Wa Sabato Tanzania
ATAPE NI NINI?
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali
Waadventista Wa Sabato
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadventista Wa Sabato Tanzania (ATAPE – Association of Tanzanian Adventist Professionals and Entrepreneurs) ni chama kilichojengwa juu ya misingi ya imani ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania kinachowaleta pamoja wanataaluma na wajasiriamali. Chama hiki kilianzishwa mwaka 1998 na kundi la wanataaluma Waadventista wa Sabato ambao waligundua kuwa ni muhimu sio tu kutumia taaluma zao kwa manufaa ya mtu binafsi bali pia kwa ajili Bwana, washiriki wenzao ndani kanisa, na jamii kwa ujumla. Kwa miaka mingi iliyofuata, kulikuwa na haja kubwa ya kuingiza wajasiriamali katika Chama. Hatimaye, mwaka 2012, uamuzi ulifanywa, na jina ATAPE lilizaliwa.
Tuna imani kwamba tutawafaikia watu wengi kupitia nawe
Uinjilisti
Afya
Elimu
Kuhamasisha washiriki wa kanisa kutumia Taaluma zao walizopewa na Mungu, Talanta na Utajiri kwa ajili ya kuboresha ustawi wa washiriki wenzao na jamii wanayoishi, na kwa ajili ya kuendeleza kazi ya injili.