Aina za Uanachama
Uanachama wa ATAPE
Kwa nini nijiunge?
- ATAPE inatoa fursa ya kipekee kwa wanachama wake kushirikiana na wataalamu na wajasiriamali wengine Waadventista wa Sabato.
- ATAPE inatoa fursa kwa wanachama wake kufanya kazi kwa pamoja kulisaidia Kanisa katika kuendeleza ujumbe wa kurudi kwa Yesu mara ya pili na kazi ya injili.
- ATAPE inawapa nguvu washiriki wake kupitia semina, makongamano, na maonyesho, na inawaandaa kutumia talanta, ustadi, na rasilimali zao kuchukua fursa zozote za biashara na za kitaaluma.
- ATAPE inatengeneza majukwaa kwa ajili ya wanachama kukutana na kubadilishana mawazo mtu mmoja mmoja au kupitia makundi. Kupitia fursa hizi za mitandao, mahusiano ya biashara ya kimkakati, ushirikiano unaoleta mabadiliko chanya na urafiki unaobadilisha maisha huundwa.
Nani anaweza kujiunga?
ATAPE inatambua Wanataaluma kama wale walio na vyeti wanaowakilisha fani walizosomea kutoka taasisi au vyuo vinavyotambuliwa na serikali. Wajasiriamali ni watu wenye uwezo wa kuona, kutambua, na kuchukua fursa zilizopo kwa faida yao wenyewe, Kanisa, na jamii inayowazunguka.
Aina za Uanachama
Hawa ni wanachama waliokidhi vigezo vya kuwa wanachama na wamekubali kujiunga na Chama kwa kulipa ada ya usajili, ada ya uanachama wa kila mwaka na michango ya kila mwaka ya uinjilisti. Hii itahusisha hata wanachama wanaoishi nje ya nchi lakini ni Watanzania wenye sifa za kuwa wanachama.
Hawa ni wanachama wote watakaopendekezwa na Kamati Kuu ya Chama na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka katika makundi yafuatayo:-
- Wanachama wa kawaida waliostaafu kazi au shughuli zao za ujasiriamali kwa umri wao na hawawezi kumudu gharama za michango.
- Watu wenye maarifa maalum na ustadi au uzoefu maalum na wanaotambulika
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Vyuo mbalimbali ambao ni Waadventista wa Sabato wataruhusiwa kuwa wanachama kwa utaratibu utakaopangwa na Kamati Kuu.