KARIBU ATAPE

Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadventista Wa Sabato Tanzania

ATAPE NI NINI?

Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali
Waadventista Wa Sabato

Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadventista Wa Sabato Tanzania (ATAPE – Association of Tanzanian Adventist Professionals and Entrepreneurs) ni chama kilichojengwa juu ya misingi ya imani ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania kinachowaleta pamoja wanataaluma na wajasiriamali.  Chama hiki kilianzishwa mwaka 1998 na kundi la wanataaluma Waadventista wa Sabato ambao waligundua kuwa ni muhimu sio tu kutumia taaluma zao kwa manufaa ya mtu binafsi bali pia kwa ajili Bwana, washiriki wenzao ndani kanisa, na jamii kwa ujumla.  Kwa miaka mingi iliyofuata, kulikuwa na haja kubwa ya kuingiza wajasiriamali katika Chama.  Hatimaye, mwaka 2012, uamuzi ulifanywa, na jina ATAPE lilizaliwa.

Huduma zaidi kwa watu wa Mungu

Mpango mkakati wa ATAPE

Jinsi ya kua mwanachama

Tuna imani kwamba tutawafaikia watu wengi kupitia nawe

JIUNGE NASI
Uinjilisti

Uinjilisti

Kusaidia ujenzi wa makanisa mapya 5 Tanzania. Kusaidia miradi ya uanzishwaji wa makanisa katika maeneo mapya
Afya

Afya

Kuendesha kambi la Afya la kitaifa katika maeneo mapya. Kusaidia na kusimamia kukamilika kwa mafanikio ya angalau miradi miwili ya uboreshaji wa vituo vya afya vya kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania
Elimu

Elimu

Kusaidia na kusimamia kukamilika kwa mafanikio ya angalau miradi miwili ya uboreshaji kwa taasisi za elimu zinazomilikiwa na kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania

Kuhamasisha washiriki wa kanisa kutumia Taaluma zao walizopewa na Mungu, Talanta na Utajiri kwa ajili ya kuboresha ustawi wa washiriki wenzao na jamii wanayoishi, na kwa ajili ya kuendeleza kazi ya injili.

KUSUDI LETU

Matukio Mapya

Habari na matukio

Kuwa mwanachama wa ATAPE

Angalia habari na matukio